HabariNews

Idara ya Usalama Mombasa Yaanzisha Harakati za Kukabiliana Uhalifu Katika Sekta ya Uchukuzi

Idara ya Usalama kaunti ya Mombasa imeanzisha harakati za kuimarisha usalama katika sekta ya uchukuzi ambayo imekuwa ikihusishwa na visa vya uhalifu katika siku za hivi karibuni.

Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Abdulrazak Jaldesa amesema kufikia sasa serikali imeweka mikakati ili kuimarisha usalama kwenye sekta hiyo  kwa kuwasajili madereva na kuwapa vitambulisho vikakavyowatambulisha.

Jaldesa amebaini kuwa wamekaa na washikadau wote wa sekta ya uchukuzi wa bodaboda, tuktuk na matatu na kukubaliana kuanza zoezi hilo kuwasajili hatua ambayo anaitaja kuwa itaondoa wahalifu wanaojificha kwenye sekta hiyo.

Miezi 2 inayokuja tunaanza mikakati imara ya kiusalama katika sekta ya tuktuk, bodaboda na matatu wote watajiandikisha na wajulikane wahudumu wote. Tumekaa na wamiliki wa sekta hizo, na tumekubaliana kuwaandikisha tujue wahudumu wa kila eneo. Wale wahalifu wanaojificha katika sekta hizo na wahudumu wasio na nidhamu tutawa flash out,” akasema Jaldesa.

Jaldesa ameongeza kuwa serikali itahakikisha kuwa vyombo vya usafiri vitakuwa na nambari ya usajili na alama ya kuonyesha eneo la kituo kinachotokea.

Vilevile Kamishna huyo amesema kuwa kutakuwa na kiongozi wa kuangalia usalama katika kila kituo ili kupunguza uhalifu unaofanyika kwa upande wa uchukuzi.

Haya yanajiri baada ya ongezeko la visa vya uhalifu kuripotiwa katika maeneo tofauti tofauti kaunti ya

BY EDITORIAL DESK