HabariMombasaNews

Wakenya washauriwa kusaka ajira Afrika badala ya kukimbilia Ulaya

Waziri wa masuala ya kigeni humu nchini Alfred Mutua amebainisha kuwa tatizo la ukosefu wa Visa litapata suluhu ya kudumu.

Akawahutubia waandishi wa habari mjini Mombasa, waziri  Mutua ametaja madeni na kuharibika kwa mitambo ya huduma hiyo kuwa changamoto kuu japo kufikia sasa hali hiyo imethibitiwa.

“ Katika shida ya paspot pia unakuta ya kwamba kuna madeni ambayo yalikuwa yako kwa muda mrefu katika serikali iliyopita ambapo wale wanaoproduce zile booklet wamesema kwamba ni lazima tuwalipe kwanza.”

Vile vile Mutua amewakemea Wakenya wanaotafuta ajira katika mataifa ya kigeni hasa Ulaya.

Kulingana na Mutua, bara la Afrika lina uwezo mkubwa wa kiuchumi.

Amesema kuna haja kwa wakenya kutafuta namna ya Kusaka ajira katika mataifa ya Afrika badala ya kukimbilia Ulaya.

BY EDITORIAL DESK.