HabariLifestyle

Raila na Ida waadhimisha miaka 50 ya Ndoa kwa sherehe Kukata na shoka

Kinara wa mrengo wa azimio Raila Odinga alimmiminia sifa mkewe Ida akisherehekea miaka 73 ya kuzaliwa kwake huku wawili hao wakiadhimisha miaka 50 katika ndoa yao.

Sherehe ya matukia haya mawili makuu ilifanyika katika mgahawa wakifahari wa Villa Rosa Kempinski ambapo wanafamilia, viongozi na marafiki wa akina Odinga walikusanyika kwa mapokezi ya kifahari.

Odinga alirejea nchini kutoka mapumzikoni Uingereza Agosti 24, 2023, kusherehekea na mkewe Ida aliyekuwa anaadhimisha miaka 73.

Katika sherehe hio ya kukata nashoka Raila alipeana sifa kedekede kwa mkewe  kwa kuwa karibu naye wakati wote, akisema ilimlazimu arejea nchini kusherehekea siku hiyo na mke wake.

“Kuolewa na wewe kwa miongo mitano kumeniletea furaha kubwa, na kusherehekea hatua hii muhimu na siku yako ya kuzaliwa ilikuwa ya kushangaza. Nisingeikosa kwa ulimwengu,” alisema.

Sherehe ya wawili hao ilipata hadhira ya baadhi ya wasanii tajika nchini akizemo Akothee na Prince Inda waliotumbuiza na kunogesha hadhira kwa miziki ya kutoa nyoka pangoni.

Wageni mashuhuri waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na kiongozi wa chama cha Narc-Kenya Martha Karua, aliyekuwa Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka, Gavana wa Siaya James Orengo, Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo miongoni mwa wengine.

BY EDITORIAL DESK