HabariLifestyleNews

Dorcas Rigathi: Wazazi wajibikieni malezi mema kupunguza uozo wa vijana mitaani

Mke wa Naibu wa rais Pasta Dorcas Rigathi ameomba wazazi kuwa na malezi mema kwa watoto wao ili kusaidia kupunguza ongezeko la vijana randaranda mtaani.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano Agosti 30, alipofungua kambi ya matibabu kwA waathiriwa wa pombe na mihadarati eneo la Shimanzi, Bi. Dorcas alisema kuwa vijana hao ni jicho la jamii hivyo ameomba wazazi kuwashika mkono kuwasaidia ili kuzuia kuwa na mawazo na kujiingiza katika kutumia miharadati.

“Sharti muwaongoze watoto wenu kwenye nia sahihi, lazima muwaongoze hasa kwenu akina mama, naongea na akina mama leo sisi ndio tunaojifungua hawa wote, hawa ni watoto wetu. Daima huwa nasema iwapo kuna mtu yeyote anayejua motto huyu ni wa nani ni mama tu,” alisema Bi. Dorcas.

Wakati huo huo Bi. Dorcas alieeleza matumaini yake kuwa vijana wanaotumia mihadarati wana uwezo mkubwa kufanya shughuli zao.

Akipigia mafano waathiriwa kutoka Mlima Kenya waliojinasua kutoka jinamizi hilo na kujitosa katika shuguli ya kuipatia kipato akieleza matumaini yake ya vijana hapa Pwani kufuata mkondo sawia.

Aidha amewahimiza vijana kuonyesha utayari wa kutelekeza mienendo potovu ili kutengeneza maisha ya mbeleni.

“Kuwa kama hivyo haimaanishi hawa ni wajinga, hawa si wajinga! Hawa ni kazi tu wanataka kupatiwa, wanataka muwapende na wanataka muwashughulikie katika ile hali ambayo imewakumba ndio waweze kuingia kwa hii mihadarati, na mkiwaonyesha njia mkiwaombea na kuwasupport mtaona watabadilika, kama kule kwetu Mt. Kenya,” akasema Bi. Dorcas.

Wakati huo huo Mwakilishi Wadi ya Shimanzi  Pricilla Mumba alieleza kuwa familia nyingi zinapitia katika hali ngumu ya maisha kwa kukosa matibabu wanapoumwa.

‘Kweli kumbe mna watu wanakumbuka na wanawapenda, mimi nikiwa nazunguka katika wadi hii nakumbana na mengi mama, na naona mengi na haswa kuna kina mama wana watoto, kuna kina mama ambao ni wagonjwa zaidi wanahitaji uangalifu wa karibu,” alisema Mumba.

Comment here