HabariNews

Ukosefu wa Ushirikiano Watajwa kudhoofisha Viwango vya Elimu Pwani

Kama njia moja ya kuimarisha viwango vya elimu ukanda wa Pwani wazazi wamehimizwa kushirikiana kikamilifu na walimu katika kufuatilia masomo ya watoto wao.

Kulingana na afisa wa maswala ya vijana kutoka shirika la Future Pillars Organisation Bilal Jokhia ukosefu wa uhusiano bora na motisha kwa wanafunzi kumechangia pakubwa matokeo duni.

Jokhia aliutaja umaskini kuwa changamoto kuu katika maswala ya elimu huku akiwataka wazazi  kuwafuatilia na kuwa na uhusiano mzuri  na walimu wa watoto wao.

Wanafuzi wenyewe hawana hima morali imekufa ,wazazi wao hawawatii moyo na walimu pia hawafanyi  kazi za ziada kumnufaisha mwanafunzi, mimi nawambia wazazim kama mwataka kutoa umaskini lazima tujukumike.”Alisema Jokhia.

Wakati huo huo Jokhia aliirai serikali kufanya juhudi zozote ili kumaliza utumizi wa dawa za kulevya akisema ndio chanzo kikubwa cha mapenzi ya jinsia moja .

Mugokaa iko na madhara kubwa sana na sana sana huchangia mapenzi ya jinsia moja ni lazima jamii ijue hili ,huu mugokaa umekuja kumaliza kizazi chetu.”Aliongeza Jokhia.

BY MEDZA MDOE