HabariNews

Gavana Achani, waziri Jumwa waongoza shughuli ya Upanzi wa miche elfu 16 Kaunti ya Kwale

kaunti ya Kwale iliandaa shughuli ya upanzi wa miche katika msitu wa kitamaduni wa kaya Lunguma, Wadi ya Tsimba Golini eneobunge la Matuga ambako miche elfu 16 ilipandwa.

Shuguli hiyo iliongozwa na Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Torathi za kitaifa Aisha Jumwa pamoja na Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani waliokuwa mstari wa mbele kuhakikisha wenyeji wa Kwale wanaendeleza upanzi wa miche.

Jumwa aliwataka wakazi wa Kwale kutokata miti kiholela kwa matumizi ya mkaa na kusisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira.

Nashkuru kwa kuungana na viongozi wa Kwale na wananchi wa Kwale kuhakikisha kwamba hii siku inafaulu. Tmepanda miti ile ambayo tulikuwatulidhamiria miche karibu elfu 16. Kukata miti ama kukata mti bila kupanda ni deni haramu, kwahivyo ni lazima tuhifadhi mazingira kivyovyote” Alisema

Kwa upande Gavana Fatuma Achani alisema kuwa serikali yake hadi kufikia sasa imepanda jumla ya miti laki 6 kwa kipindi cha mwaka mmoja katika maeneo Mbali mbali ya kaunti ya hiyo na kusema kuwa wanalenga kupanda miti laki moja kuanzia Januari mwaka ujao.

Gavana Achani aidha aliwahimiza wakazi wa Kwale kulinda mazingira pamoja na kupanda miti hadi majumbani mwao ili kuhakikisha kuwa wakazi wanapata chakula cha kutosha kutokana na uwepo wa mvua ya kutosha kwa sababu ya miti.

Hii kaya kama mvua inanyesha vizuri ukilima mahindi vinaendana. Suluhisho la kusema nakata kwa sababu nina njaa si suluhisho, ni sisi na nyinyi tushirikiane tuhakikishe tunaleta njia mbadala ya kuhakikisha mwananchi anafaidika. Mimi yangu tu nikuwahimiza watu tuendeleeni kupanda miti,” alisisitiza

BY BINTI HAMISI