HabariNews

Kizaazaa Bandarini, KPA yategua kitendawili cha umiliki wa Meli ya Mafuta

Mamlaka ya Bandari ya Mombasa KPA imejitoa kimasomaso kukana madai kuwa Anne Njeri Njoroge ndiye mmiliki wa meli ya mafuta iliyotia nanga bandarini humo.

Kwenye kikao na waandishi wa habari KPA ilipuuzilia mbali kwamba mwanabiashara huyo ni mmiliki wa meli hiyo ya shehena ya mafuta inayogharimu takribani bilioni 17, bali inamilikiwa na Aramco.

Meli hiyo ya mafuta ya Dizeli ni moja ya mpango wa kuagiza mafuta kutoka serikali kwa serikali (G2G) na wala si kupitia kwa wafanyabiashara wa kibinafsi.

Captain William Ruto ni Meneja Mkurugenzi wa KPA na alieleza haya.

 

Sisi hatujawahi kuonana na mtu anaitwa Anne, na wala hajawahi kufika ofisi zetu za KPA kulaunch any complain kwetu. Sababu mtu unajua kama meli inakuja Bandari ya Mombasa na KPA ndio inasimamia bandari ya Mombasa, ungekuja hapa ukatuelezea na tukaangalia kama kweli mzigo ni wako, so hiyo mambo ya Anne hatujui,” alisema Captain Ruto.

KPA ilibaini kuwa meli hiyo iliwasili nchini tarehe 4 mwezi Novemba ikiwa na tani 93,460.46 ya mafuta ikitokea Saudi Arabia na wala sio Azerbaijan kama ilivyodaiwa.

Kulingana na stakabadhi ambazo KPA iko nazo tani elfu 49,091 ni za hapa nchini, na tani elfu 44,369 zikiwa za Uganda, Sudan Kusini na DR KONGO na kampuni ya mwanabiashara huyo Annes imports haikuwa na mzigo wowote katika meli hiyo.

 

Kati ya sheheha hizo tani 93,460 za mafuta, tani elfu 49 zilikuwa za hapa nchini na mwenye shehena hiyo ikiwa kampuni ya MS Armco Trading, Fujaira kama ilivyoteuliwa na Wizara ya kawi na Mafuta na tani zilizosalia za elfu 44,369 zilikuwa za mataifa Jirani ikiwemo Uganda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwa hiyo ukiona hapa stakabadhi hizi hapa juu shipper ni yeye, consignee ni yeye third party na kila kitu ni yeye, hizo ni story za jaba,” alisema Benjamini Tayari, Mwenyekiti wa Bandari ya Mombasa, KPA.

Mfanyabishara huyo ambaye kwa sasa ametoweka hajulikani kule aliko huku Waziri wa Kawi Davis Chirchir akikiri na kuthibitisha kuwa mfanyabishara huyo aliwahi kufika ofisini kwake.

Na Japo hakufichua kiini cha Anne kuzuru ofisini kwake, Waziri Chirchir alisisitiza kuwa sheheha ya mafuta ya dizeli ambayo mfanyabishara huyo alidai kuwa yake ni ya Galana Energies moja ya kampuni zilizopewa kandarasi kuleta mafuta nchini katika mpango baina Kenya na mataifa ya Arabuni.

Hiyo kesi iko kortini kwa sasa, nafahamu mwanamke anayeitwa Anne alikuja ofisini kwangu ameenda huko kwa Port akasema meli ni yake. Hiyo meli ilifika kitambo brought in by a company inaitwa Galana na has been discharged, so tutashirikiana kujua ukweli uko wapi, lakini kesi iko kortini kwa sasa.” Alisema.

Kwa sasa mawakili wa mfanyabishara huyo Anne Njoroge, wamesema mteja wao hajulikani aliko huku wakidai kuwa mara ya mwisho kuongea naye ilikuwa siku aliyofika makao makuu ya upelelezi nchini DCI kuandikisha taarifa.

BY MJOMBA RASHID

Comment here