HabariNews

Waziri wa uchukuzi Kipchumba Murkomen Awaongoza Wakazi Mombasa katika zoezi la Upanzi wa Miche

Waziri wa uchukuzi na barabara Kipchumba Murkomen pamoja na viongozi wa kaunti ya Mombasa wamewaongoza wakaazi wa kaunti hiyo katika zoezi la upanizi wa miti maeneo ya Ganahola eneobunge la Jomvu.

Kulingana na Murkomen takribani miche billion 15 inayolengwa na serikali kwa kipindi cha mika 10 ijayo kupandwa kote nchini kaunti ya Mombasa itashughudia upanzi huo kwa kupanda miche zaidi ya million 7 kulingana na maono ya serikali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini.

Waziri huyo alitoa changamoto wakaazi wa kaunti ya Mombasa kuilinda na kuitunza miti hiyo ili iwafaidi katika siku za usoni pasi na kuiachilia bila kuwa waangalifu nayo alisema hatua ni yakipekee ya kusaidia  kukabiliana na mumomonyoko wa ardhi.

Nia yetu kama serikali ni kupanda miche ya miti takribani billion 15.9 ifikapo mwaka 2032 na nafuahi katika kaunti ya Mombasa tumeweza kupanda miche 30,000 na hii inaonyesha tunaelekea pazuri kama serikali na nimeona watu wengi wamejitokeza ili kuapnda mikoko mahali hapa.Hivyo tuitunze miti yetu kwa manufaa yetu ya baadae”.Alisema Murkomen.

Murkomen aidha aliisifia Ustawisajiwa miti ya mikoko akiitaja hususan kwa sifa yake ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi akisema iko na uwezo kubwa wa kukabiliana na mumomonyoko wa udongo na hali ya hewa.

Katika miti  yote mkoko uko mstari wa mbele kwa kulinda mazingira na kukabiliana na hali ya tabia nchi, hivyo nivuzuri kuekeza katika mti huu kwa uwezo ulionao kwa mazingira yetu”.Alisistiza Murkomen.

Wazuri  Murkomen aliwahimiza wakenya kuungana katika zoezi hilo ili ifikapo mwezi Disemba wawe wamefikia asilia 30 la upanzi wa miche.

EDITORIAL DESK