HabariNews

Kenya inaelekea pabaya! Utafiti wa InfoTrack Wabaini

Wakenya 6 kati ya 10 wanaamini kuwa taifa limechukua mkondo mbaya na linaelekea kusikostahili.

Haya ni kwa mujibu wa Utafiti wa hivi punde uliofanywa na shiirka la InfoTrack.

Idadi hiyo imeongezeka ikilinganishwa na idadi ya mwaka jana ambapo asilimia 55 ya Wakenya waliohojiwa ndio walioamini kwamba Kenya inaelekea mkondo mbaya.

Utafiti wa Info Track unaonyesha kwamba Wakenya kutoka pembe zote za taifa hawajaridhishwa na jinsi taifa linavyoendeshwa wakiongozwa na wenyeji wa Nyanza kwa kiwangoi cha asilimia 72 kisha magharibi mwa kenya kwa asilimia 69.

Katika utendakazi rais William Ruto amepata asilimia 47 ambayo ni na alama ya D naye naibu wa rais Rigathi Gachagua akizoa alama ya E sawia na asilimia 36.

Baraza la Mawaziri, wabunge, idara ya mahakama na serikli za kaunti wote wakipewa alama ya D katika utendakazi wao.

Ripoti hiyo aidha imebaini kuwa Asilimia 30 ya Wakenya ingali katika matumaini kuwa maisha yataimarika mwaka ujao huku asilimia sawa na hiyo ikisema kuwa hali itasalia ilivyo na asilimia 16 ikisema hali itazidi kuwa mbaya.

Utafiti huu wa Info Track ulifanywa kati ya tarehe 18 na tarehe 19 mwezi wa Disemba na ulihusisha jumla ya Wakenya 1500 katika kaunti zote 47.

BY EDITORIAL DESK