HabariNews

Ada mpya za Nauli zilizoongezwa katika garimoshi la kisasa

Ada mpya za Nauli zilizoongezwa katika garimoshi la kisasa, SGR zimeanza kutekelezwa rasmi kuanzia Januari Mosi.

Kwa sasa safari kutoka hapa mjini Mombasa hadi jijini Nairobi ni shilingi 1,500 kutoka shilingi 1,000 kwa mabogi ya kawaida (economy class).

Kwa wanaosafiri katika bogi la kwanza (first class) kutoka Mombasa hadi Nairobi, sasa watalipa shilingi 4,500 ada hiyo ikiwa imeongezeka kutoka shilingi 3,000.

Malipo ya nauli ya kawaida kutoka kutoka kituo cha mjini Miritini mjini Mombasa hadi Voi ni 440, Mombasa hadi Miasenyi ni 290 na Mombasa-Mariakani ni shilingi 110.

BY MJOMBA RASHID