HabariNews

Gharama zaidi! Serikali yaongeza ada kwa watumiaji wa Barabara ya Nairobi Expressway

Serikali imeongeza ada zinazotozwa katika kutumia Barabara ya moja kwa moja inayopita kwa juu ya Nairobi Expressway.

Magari yanayotumia Barabara hiyo yaliyokuwa yakitozwa shilingi 100 kutumia Barabara hiyo sasa yatalipa shilingi 170 na yale yaliyokuwa yakilipa shilingi 310 yatalipa shilingi 500.

Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen ametangaza nyongeza ya ada hizo na kwamba tayari zinaanza kutozwa mara moja baada ya kuchaopishwa kwenye gazeti rasmi la Serikali la Disemba 31, 2023.

“Katika kutekeleza mamlaka yaliyotolewa na kifungu cha 4B (3) cha Sheria ya Ushuru wa Barabara za Umma, Waziri wa Barabara na Uchukuzi anaidhinisha viwngo vya ushuru vya Barabara ya Nairobi Express Way kama ilivyobainishwa karika Ratiba hiyo,” ilisema Notisi hiyo.

Waziri Murkomen alisema nyongeza hiyo ni kutokana na viwango vya mabadiliko ya dola kote duniani.

Katika viwango vipya vya ada, Wendeshaji magari wanaoingia Barabara hiyo kwenye kituo cha Mlolongo na kutokea katika kituo cha SGR na Eastern Bypass watahitajika kulipa shilingi 250 kutoka shilingi 100 ya sasa na wale watakaokuwa wakitoka katika barabara hiyo kwenye kituo cha Southern Bypass watalipa shilingi 330 kutoka shilingi 210.

Katika njia iyo hiyo, magari yanayotoka katika vituo vya Capital Hill na Haile Selassie watalipa shilingi 410 kutoka shilingi 210.

Na kwa magari yatakayotokea katika vituo vya Museaum Hill, The Mall na Westland watalipia shilingi 500 kiwango kilichopanda kutoka shilingi 310.

Njia fupi ya kutoka Syokimau hadi kituo cha SGR na vile vituo vya SGT na JKIA kuelekea Eastern Bypass vitagharimu madereva shilingi 170 kutoka shilingi 100 ya hapo awali; ada ambazo zitatumika pia kinyume chake.

Ikumbukwe kuwa ada hizi mpya zinatekelezwa kwa vituo vyote vya Barabara hiyo kutoka Mlolongo hadi Westlands jijini Nairobi, kuenda na kurejea.

BY MJOMBA RASHID