HabariNews

Shida ya Kenya si ushuru tunaotoza, shida kubwa ni Madeni! Asema Rais Ruto

Changamoto kuu na shida zinazokabili nchi hii ni Madeni na wala kodi na ushuru unaotozwa.

Hii ni kauli yake rais William Ruto, akizungumza huko kaunti ya Nyandarua.

Rais alibaini kuwa serikali yake imelazimika kusitisha baadhi ya shughuli ili kuhakikisha inapunguza madeni yake inayodaiwa.

Ruto amesema kuwa licha ya lawama zinazoelekezewa serikali yake katika utozaji wa ushuru, ukweli utasalia kuwa malimbikizi ya madeni ndiyo yanayolemaza mataifa mengi barani Afrika na kote ulimwenguni.

“Kuna mjadala mkubwa watu wanasema wanajaribu kulaumu kwamba shida ya Kenya ni ushuru, wacha niwaambie ukweli ya kwamba shida ya Kenya si ushuru shida ya Kenya ni madeni. Alisema rais.

Na huo ndio, ukweli kuna watu hawataki kuambiwa ukweli, na hii madeni ndiyo imesababisha nchi zingine nyingi hapa bara la Afrika wakakosa kulipa madeni yao saa hizi wako katika janga hawajui watatoka katika kwa njia gani.” Alisema.

Wakati uo huo rais ametaja watangulizi wake kama aliyekuwa rais wa 3 nchini hayati Mwai Kibaki kuwa alifanikiwa kukuza Uchumi wa nchini kupitia ukusanyaji ushuru na mapato.

“Mataifa mengi yaliyoendelea yamejengwa kwa ushuru wao wenyewe na huko ndiko tunafaa kuelekea na hiyo ni ukweli lazima tuambiane polepole.” Alisema.

Kauli yake kiongozi wa taifa iliungwa mkono na Spika wa bunge la Seneti Amason Jeffa Kingi ambaye amekariri kuwa mikopo inayochukuliwa na nchi ni sawa na ushuru ulioahirishwa na ambao ni lazima ulipwe kwa gharama yoyote ile.

BY MJOMBA RASHID