HabariLifestyleMombasaNews

Wadau wa Utalii Kilifi Wapinga Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Kawi ya Nuclear

Wadau wa sekta Utalii Kaunti ya Kilifi wamepinga vikali ujenzi kiwanda cha uzalishaji wa kawi ya Nuclear katika eneo la Uyombo wadi wa Matsangoni.

Wakiongozwa na  Michael Changawa wadau hao kutoka eneo la Watamu wamesema ujenzi wa kiwanda hicho utaathiri pakubwa biashara zao pamoja na mazingira ya wakazi eneo hilo.

Aidha wakazi hao wameshikilia kuwa huenda mandhari ya bahari ambayo ni kivutio cha utalii yakachafuka na hivyo kuhatarisha viumbe hai wa bahari wakiwemo nyangumi ambao ni kivutio kikuu cha utalii.

“Kituo hicho kitakuwa na hatari hasa kwa viumbe vya bahari ambavyo kwetu sisi ni muhimu kama wakaazi na kivutio cha wageni kwa hivyo hiyo itaharibu ile mazingira kwetu ambao huo mradi unafaa kufanywa.” Alisema.

Kwa upande wake seneta wa Busia Okiya Omtata amewataka wakaazi eneo hilo kufutilia mbali kesi iliyoko mahakamni na kulipa nafasi Bunge la Seneti kuingilia kati na kufanya kazi yake iwapo wanataka usaidizi na haki kupitia bunge.

“Wananchi ndio wenye mamlaka kwa sababu ndio walituchagua sasa tumerudisha kwao wachague kama wanataka bunge ni sawa na mimi ningewambia waondoe ile hoja kotini kwa sababu ina nafasi ya baada ya bunge kuenda mahakamani lakini wakienda mahakamani hawana nafasi ya kurudi bunge.” Alisema Omtata.

Naye mkurugenzi Mkuu wa Shirika la mazingira la Centre for Justice Governance and Environmental Action, Phyillis Omindo amesema kesi iliyowasilishwa mahakamani inafutiliwa mbali iwapo bunge la seneti litahakikisha wakaazi watapata haki.

“kama jamii tumejua kuna kesi na tunaenda kuweka saini ya kusema kuwa sisi watu wa Uyombo hatuhusiki na kesi hiyo kwa sababu haijulikani ni nani ameeka wakili wao akiulizwa anasema hawezi kuweka wazi watu hao.” Alisema Omido.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la NUPEA, Justus Wabuyabu amebainisha kuwa shirika hilo litazidi kushirikiana na jamii kuhakikisha wanahamasishwa vilivyo kuhusu umuhimu wa mradi huo.

BY MEDZA MDOE