HabariLifestyleMombasaNews

Mackenzie Aitaka Mahakama Kupunguza mashtaka Yanayomkabili hadi 12 Pekee

Mawakili wa mshukiwa mhubiri tata Paul Mackenzi wamelalamikia suala la mteja wao kuongezewa mashtaka wanayodai kutokuwa haki.

Mawakili hao wametaka mahakama kuu kufutilia mbali stakabadhi za mashtaka zaidi ya 190 iliyowasilishwa dhidi ya Mackenzie na washukiwa wenza wakidai ni kinyume Cha sheria na kupendekeza kupunguzwa hadi mashtaka 12.

Wakiongozwa na Wicliff Makasembo na James Mouko, mawakili hao wanasema mahakama kuu na ile ya upeo ina mamlaka kusikiliza mashtaka 12 pekee kwani idadi ya mashtaka waliyowekewa mteja wao na washukiwa wengine ni ya kushtua.

Wanasema mashtaka yote yanafanana kwani ni ya mauwaji japo hayaelezi jina, umri wa waathiriwa na mahali mauwaji hayo yalitekelezwa na kuitaka mahakama kutupilia mbali mashtaka hayo.

Aidha viongozi wa mashtaka wakiongozwa na Victor Mule, wameyapuuzilia mbali maombi ya mawakili hao wakisema kunao ushahidi wa mashtaka zaidi ya 12 ya kusikilizwa na kuamua.

Wameitaka mahakama hiyo kutupilia mbali maombi na kuendelea na kesi hiyo.

Upande wa mashtaka vile vile umeonesha nia ya kuitaka mahakama kutoa hukumu ya kinyongo Kwa washukiwa japo unafahamu kuwa Kwa Sasa hukumu hiyo iliondolewa.

BY JOSPEH YERI