HabariLifestyleMombasaNews

Mbunge wa Rabai Anthony Kenga Akashifiwa Vibaya na Wanamazingi Pwani.

Wanamazingira ukanda wa Pwani wamekashifu hatua ya mbunge wa Rabai Anthony Kenga Mupe kwa madai ya kukata miti eneo la Mwawesa Kaunti ya Kilifi ili kupisha ujenzi wa kiwanja.

Wakiongozwa na Dkt Edwin Muinga Chokwe ambaye ni mwanaharakati wa mazingira kutoka shirika la Clean Mombasa alisema jambo hilo linahatarisha juhudi za utunzaji mazingira pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha Muinga alisema inasikitisha kuona kuwa licha serikali kupigania upanzi wa miti ili kuongeza idadi ya misitu humu bado kuna watu hasa viongozi wanaojihusisha na ukataji wa miti Kkiholela.

“Ni jambo ambalo limetuhuzunisha wakereketwa wa mazingira ha sa wakati huu ambapo tuna mambo ya mabadiliko ya tabia nchini na zamani miti ilikatwa kwa sababu ya kazi tofauti ikiwemo biashara ya makaa lakini sasa baada ya kufahamu athari zake inakuwa ni sikitiko kubw hasa kama mtu ni kiongozi.” Alisema Muinga

Muinga alifichua kuwa hadi kufikia sasa hawajapata taarifa iwapo jambo hilo lilitekelezwa kisheria licha ya kuhusisha asasi mbali mbali wakiwemo maafisa wa kulinda misitu huku akidai kuwa huenda jambo hilo limefanywa kisiri baina ya mbunge huyo na naibu Chifu wa eneo na sasa akitaka lisitishwe mara moja.

“Mimi nimezungumza na afisa wa msitu wa Kilifi Bw Fondo na vile vile yule wa Mombasa na amesema hana habari kwa hivyo inaonekana ni kitu kinfanywa chini chini kati ya mbunge na Naibu chifu na sasa tumekemea hili jambo na lisitishwe mara moja na zaidi sisi wanaharakati turudi tupande miti pale.” Alinena Muinga

Hata hivyo Muinga alitishia kuhusisha jamii kumchukulia hatua kiongozi huyo akidai huenda akachukua fursa hiyo kuendeleza ukataji miti kwa manufaa yake bali sio maendeleo ya jamii.

“Itatubidi sisi tuchukua hatua za kisheria na tunaogopa akianza kukata kaya moja atakata kaya zote na sisi tunaamini kuwa ata sio kujenga anataka kujenga labda anataka nafasi ya kunyakua kwa hivyo lazima tuende mbio sana na wananchi wahusishwe.” Alisema Muinga

BY EDITORIAL DESK.