HabariKimataifa

TETEMEKO AFGHANISTAN LIMESABABISHA WATU KUJEHURIWA HUKU WENGINE WAKIPOTEZA MAISHA.

Maafisa wa Taliban wamesema kuwa Tetemeko kubwa la ardhi limesababisha vifo vya takriban watu 920 na wengine kadhaa kujeruhiwa mashariki mwa mkoa wa Paktika, nchini Afghanistan.

Kiongozi wa Taliban Hibatullah Akhundzada amesema mamia ya nyumba zimeharibiwa na huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Naibu waziri wa usimamizi wa majanga Sharafuddin Muslim aliambia mkutano wa wanahabari kuwa takriban watu 920 wameuawa na wengine 600 kujeruhiwa.

Tetemeko hilo lilipiga takriban kilomita 44 kutoka mji wa kusini-mashariki wa Khost wakati wa usiku.

Katika maeneo ya mbali, helikopta zimekuwa zikisafirisha waathiriwa hadi hospitalini.

Maafisa wa Taliban wametoa wito kwa mashirika ya misaada kukimbilia katika maeneo yaliyoathiriwa mashariki mwa taifa hilo.

>> News Desk…