AfyaHabariLifestyleMombasaNewsSiasa

Jamhuri Dei spesheli: Fatma Kushe ataka kutengwe vyumba maalum gerezani kwa Wake kukutana na Waume wao kimapenzi

Mwakilishi Wadi ya Kadzandani eneobunge la Nyali Fatuma Swaleh Mote amependekeza kufanywe marekebisho ya sheria kuwaruhusu wafungwa kutangamana na wachumba wao magerezani kama njia mojawapo ya kupunguza visa vya ulawiti na ushoga katika jela.

Mwakilishi wadi huyo wa Kadzandani maarufu Fatuma Kushe akiwa ameandamana na Gavana wa kaunti ya Mombasa aliibua hoja hiyo katika maadhimisho spesheli ya sikukuu ya Jamhuri huko katika taasisi ya Jela Baridi wakati wa kuachia huru wafungwa wa makosa madogo madogo.

Bi. Kushe anataka sheria ipitishwe ya kuwaaruhusu wafungwa kutangamana na wachumba wao gerezani lengo kuu likiwa ni kupunguza visa vya ulawiti na mapenzi ya jinsia moja katika magereza hayo.

“ikiwa kuna mwanamume ama mfungwa amefungwa zaidi ya miaka 2 waweze kutenga vyumba maalum, na mimi najua mwanamume hawezi kujizuia, watu wakitoka hapa unasikia mwanamume anafanya mapenzi ya jinsia moja, mashoga wanaongezeka kwa sababu huku hawapati burudani.

Naiomba Serikali ikiwa iweze kutenga sehemu maalum mtu akishikwa mke wake aweze kumtembelea maanake hawezi kujizuia na hawapati burudani la tendo,” alisema Bi Kushe.

Diwani huyo kadhalika alisema familia nyingi za wafungwa zimevunjika na kusambaratika kutokana na baadhi wa wafungwa kuwekwa ndani kwa kipindi kirefu bila kutangamana na wachumba wao.

Fatuma swaleh sasa anaitaka serikali kuifanyia sheria marekebisho na kubuni vipengee maalum vitakavyofanikisha wito na kauli yake.

“Vijana wale wetu wadogo mto ameoa amefanya makosa amekuja kufungwa anawekwa miaka 5 akitoka hapo mke amemkimbia hajua aanze vipi, lakini wangetupa nafasi kina mama kuja kutembelea waume zetu kule Ughaibuni vitengo kama hivyo viko lakini Kenya hatuna.

Namuomba rais wetu wa Kenya yeye ana uwezo atufanyie haya ili tuje tuburudike na waume zetu ndani ya magereza,” alisema.

Kauli ya Diwani huyo inajiiri huku madai ya ulawiti magerezani yakiripotiwa na kwa mujibu wa Fatuma Mote hii ni mojwapo ya njia ya kudhibiti visa hivyo.

BY MJOMBA RASHID