HabariMazingiraNews

VIONGOZI WA KWALE WAHIMIZWA KUMALIZIA MIRADI ILIOANZISHWA.

Mbunge wa Kinango Samuel Gonzi Rai amewataka viongozi walioingia madarakani katika eneo bunge hilo kukamilisha miradi mbalimbali iliyoanzishwa na viongozi waliotoka ili kufanikisha ajenda ya kukuza maendeleo katika eneo bunge hilo.

Akizungumza katika shule ya msingi ya Kinango wakati wa ziara ya kutathmini miradi ambayo haijakamilika Gonzi amesema kuwa ni muhimu kwa kila kiongozi anayechukua usukani kukamilisha miradi kwa manufaa ya mwananchi.

Gonzi amesisiza haja ya wanasiasa kuweka  kando tofauti zao za kisiasa akisema kuwa kuendeleza kupiga siasa hakutasaidia wakaazi kupata maendeleo wanayostahili.

Mbunge huyo hata hivyo ameahidi kukamilisha miradi iliyoanzishwa na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Benjamin Tayari ili kubadilisha sura ya eneo la eneo bunge hilo.