HabariMazingiraNews

Wanamazingira Pwani wapongeza Mahakama Kubatilisha Agizo la Rais la Ukataji miti

Wanaharakati wa Mazingira Pwani wamepongeza hatua ya Mahakama kubatilisha agizo la rais William Ruto la kuruhusu ukataji na usafirishaji wa miti.

Mahakama ya Mazingira na Ardhi ilipiga marufuku ukataji wa miti hatua ambayo imeungwa mkono na wanamazingira ikizingatiwa kuwa ukataji miti unaleta athari kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi sawia na uharibifu wa mazingira.

Bosco John Juma ambaye ni Mwanamazingira eneo la Pwani kutoka Shirika la Big Ship amesema marufuku hiyo itaipa miti nafasi ya kukomaa na kurudisha asili yake huku akitaja kuwa uharubifu sana sana unachangiwa na wanaokata miti kupata mbao na hata kutengeneza makaa.

“Watu wakipata nafasi tu kidogo kama hiyo ukataji miti unakosa kusimamiwa vizuri. Kwa sababu tuko na hioy ban on illegal logging, lakini twashuhudiwa watu wa pikipiki kutoka Bamba, Kaloleni wakileta makaa kuuza mijini na hiyo ni hatari kubwa itakapoondolewa marufuku hiyo basi uhalifu unafanyika,” alisema Bw. Bosco.

Vile vile Bosco amekashifu ukataji wa mibuyu unaoendelea na kusema kuwa ukataji miti unapoteza asili ya nchi hususan miti ya mibuyu ambayo hupanitakana sehemu hasa za Pwani.

“Kuzuiliwa kwa ukataji miti ni vyema sana na suala la kukatwa kwa miti ya mibuyu nalikemea vikali, tunapoteza asili ya nchi miti ikiangamia kwani sin chi zote zina mibuyu hapa Afrika,” alisema.

Ikumbukwe kuwa Rais William Ruto aliweka bayana kuwa amri yake ya kuondoa kwa marufuku ya ukataji miti ni kwa nia njema ya kutoruhusu bidhaa za miti kuendelea kuharibika misituni kutokana na kusalia huko muda mrefo kufuatia agizo la kutoruhusu ukataji miti.

“Niliambia wale watu, ile Korti iko pale pia iheshimu ile kazi tunafanya. Hatutaruhusu miti yetu iharibike msituni na ilhali tunaweza kuitumia kukuza uchumi wetu, hatutaagiza fanicha nje ya nchi,” alisema rais Ruto.

Hata hivyo Kiongozi huyo wa nchi alibainisha kuwa kuagiza kurejelea ukataji miti, hakumaanisha kuwa kila mmoja aliruhusiwa kukata miti ovyo.

“Tukisema ya kwamba tutaendelea na kuvuna bidhaa za msitu hiyo haimaanishi kuwa misitu itakuwa inakatwa kiholela, hiyo haiwezi kufanyika so kama kuna mtu alikuwa anafikiri sasa iko licence ya kukata miti left right and centre utakutana na sisi. Sikizeni vizuri mambo ya kuvamia misitu will not happen, tunaelewana? Hakuna kuvamia misitu.” Alibainisha rais.

Na Mjomba Rashid